July 15, 2017Kikosi cha Taifa Stars kimeshindwa kuonyesha cheche katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu Chan baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Rwanda.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wageni Rwanda walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza baada ya kupasiana vema kuingia katika lango la Stars.

Stars ilionekana kucharruka na kuwapa wakati mgumu Rwanda au Amavubi kabla ya kupata bao la kusawazisha kupitia nahodha Himid Mao katika dakika ya 34.

Beki wa kushoto, Gardiel Michael aliachia mkwaju mkali na beki mmoja wa Amavubi wakati akiokoa, aliunawa na mwamuzi akasema ni tuta.


Matumaini makubwa yalikuwa katika kipindi cha pili lakini Stars ilishindwa kuonyesha kabisa cheche zake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV