July 11, 2017


Pamoja na uongozi wa Simba kutumia nguvu nyingi kuonyesha bado uko na Jackson Mayanja, kocha Niyongabo Amars amesema wanaendelea na mazungumzo.

Amars ambaye ni kocha msaidizi wa zamani wa timu ya taifa ya Burundi amesema wako katika hatua nzuri.

“Kweli ninaweza kuja Simba na tumezungumza. Tumemaliza mambo mengi ya kimsingi,” alisema.

“Hili ni suala la makubaliano, nikiona sawa na wao wakiona sawa nitakuja. Ikiwa tofauti basi halitakuwa jambo baya kutokuja.”

Baada ya taarifa za Simba kufanya mazungumzo na kufikia katika hatua nzuri na Amars, taarifa zilieleza Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog aliweka msisitizo kwamba angependa kufanya kazi na Mayanja.

“Sasa hapo ndiyo kumekuwa na mkanganyiko lakini wako wanaosisitiza lazima Mayanja amuachie kocha Mrundi,” kilieleza chanzo.


Baada ya kauli ya Omog, Simba imekuwa ikijitahidi kusambaza picha za Mayanja akiwa mazoezini kama kuonyesha hakukuwa na mazungumzo au mpango wowote na kocha huyo Mrundi anayesifiwa kwa kusimamia nidhamu na viwango vya wachezaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV