July 11, 2017


Kocha Mkuu wa Everton, Ronald Koeman amesema kila mchezaji aliyesafiri kuja Tanzania akiwemo Wayne Rooney atacheza kwa dakika 45 katika mechi dhidi ya Gor Mahia.
Tayari kikosi cha Everton kiko angani kuitafuta Dar es Salaam.
Everton itawavaa Mabingwa wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Koeman amesema atafanya hivyo kutoa nafasi kwa kila mchezaji aliyesafiri kupata nafasi ya kucheza.
“Hii ni sehemu ya maandalizi na itakuwa ni vizuri kila mmoja apate nafasi ya mazoezi kwa kucheza mechi hiyo,” alisema.

Rooney amejiunga tena na Everton siku tatu zilizopita akitokea Man United ambayo alijiunga nayo miaka 13 iliyopita akitokea Everton.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV