July 8, 2017
Athanas Michael ambaye ameshindwa kupata namba ya uhakika Simba ametua Singida United kwa mkataba wa miaka miwili na Kocha Mkuu, Hans van Der Pluijm anatamba kuwa atawashangaza.

Pluijm raia wa Uholanzi anasema Athanas ambaye alianza kuonyesha cheche akiwa Stand United, atawashangaza wengi.

Pastory hivi karibuni alitangazwa kusajiliwa kwa mkopo na Singida United kisha akakabidhiwa jezi kwa ajili ya kuichezea timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji huyo alikuwemo katika orodha ya wachezaji wa Simba waliopangwa kutolewa kwa mkopo akiwa ameichezea Simba kwa miezi sita pekee tangu asajiliwe.

Pluijm alisema anafahamu uwezo mkubwa wa Pastory, hivyo anaamini ujio wake utaimarisha kikosi chake kwenye safu ya ushambuliaji.

“Mimi ndiye niliyependekeza usajili wa Pastory baada ya kuvutiwa na kiwango chake ndani ya uwanja na ni hatari kwenye lango la wapinzani.

“Hivyo basi, nikatoa pendekezo kwa viongozi wangu ili tufanikishe mpango huo wa kumsajili baada ya kuona Simba hawana mpango naye,” alisema Pluijm.


“Naamini Pastory atazifunga sana timu pinzani tutakazokutana nazo na hii itadhihirisha ubora wake ndani ya uwanja, ni jambo la kusubiri muda ufike tu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV