July 8, 2017Unaweza kusema kwa asilimia 80 sasa, Mshambuliaji nyota nchini England, Wayne Rooney atakuwa katika msafara wa Everton utakaokuja nchini siku mbili zijazo.

Everton inakuja nchini kucheza na Mabingwa wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia, mechi itakayopigwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Leo mchana, Rooney amewasili makao makuu ya Everton kwa ajili ya kufanya vipimo.

Rooney amekubali kurejea nyumbani Everton baada ya Manchester United kumsajili Romelu Lukaku ambaye itamtangaza ndani ya siku moja.

Rooney amekubali kurejea nyumbani Everton baada ya Manchester United kumsajili Romelu Lukaku ambaye itamtangaza ndani ya siku moja.

Kitendo cha Rooney kutua na kufanya vipimo maana yake kila kitu kimekamilika na sasa atakuwa kati ya wale watakaokuja Tanzania.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV