July 8, 2017


Kamati mpya ya Uchaguzi wa TFF, imetangaza majina ya wagombea waliopita usaili huku Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiondolewa.

Kuondolewa kwa Malinzi, maana yake hataweza kushiriki uchaguzi huo ambao awali ulipangwa kufanyika Julai 12 kabla ya mchakato wake kusitishwa kwa muda.
Kamati hiyo inayoendelea kuongozwa na wakili Revocatus Kuuli ambaye alikuwa na msimamo uliosababisha wajumbe wanne wa awali kuondolewa, imemuondoa Malinzi kwa kuwa ameshindwa kutokea katokea katika usaili.

Malinzi hakutokea katika usaili kwa kuwa yuko mahabusu akituhumiwa na makosa zaidi ya 20 yakiwemo yale ya matumizi mabaya ya ofisi na uhujumu uchumi.

Awali, wajumbe walitaka kuhakikisha anasailiwa hata kupitia karatasi zake tu, jambo ambalo lilipingwa na Kuuli ambaye alisisitiza kila anayesailiwa lazima atokee mwenyewe.

Wengine walioenguliwa katika nafasi hiyo ya urais ni John Kijumbe, Frederick Msolwa pia.

Kuondolewa kwa Malinzi, maana yake wagombea wa Urais TFF wanabaki kuwa ni Shija Richard, Imani madega, Ally Mayay, Wallace Karia na Emmanuel Kimbe.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV