July 10, 2017

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, DK. Harrison Mwakyembe amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi pamoja na wajumbe wote wa baraza hilo.

Dioniz Malinzi
Waziri Mwakyembe amechukua uamuzi huo leo Jumatatu katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kufuatia agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati wa hotuba yake ya kufunga bunge, kuvunjwa kwa BMT kama haitaonekana  kuwa na utendaji mzuri.

Licha ya kusitisha uteuzi wa mwenyekiti wa baraza hilo waziri hiyo pia amesitisha uteuzi wa wajumbe wote katika baraza hilo huku sekretarieti ikipewa jukumu la kuendelea na kazi zake kwa kushirikiana na serikali wakati ikijipanga kwa ajili kuanza mchakato wa kutafuta viongozi wapya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV