July 10, 2017Kiungo wa zamani wa Simba, Pierre Kwizera amebeba tuzo wa mwanasoka bora wa Rwanda kwa msimu wa pili mfululizo.

Kwizera sasa anaichezea Rayon Sports aliyojiunga nayo akitokea Simba ambako alionekana hafai.

Mrundi huyo ambaye ana pasi za rula, amekuwa gumzo tokea alivyotua Rwanda na kuisaidia Rayon Sports kuzima utawala wa mfululizo wa APR inayomilikiwa na jeshi la nchi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV