August 7, 2017Neymar dos Santos ambaye ni mchezaji ghali zaidi duniani, ameamua “kujiachia” kabla ya kuanza kazi yake rasmi.

Mshambulizi huyo raia wa Brazil, ameamua kusafiri hadi Kusini mwa Ufaransa, eneo liitwalo St Tripez kula bata akiwa na rundi la marafiki zake wakiwa katika boti ya kifahari.


Ameamua kula bata akijiandaa kuanza kuichezea Paris Saint-Germain kwa mara ya kwanza.

Amejiunga na PSG kwa kitita cha pauni milioni 198 ambazo zinamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kwa kipindi hiki.

Neymar alionekana ni mwenye furaha akiwa na rafiki zake hao.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV