August 10, 2017
Baba mzazi wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Saimon Msuva amesema fedha yote ya usajili ya kwanza kabisa ya mwanaye waliipeleka kanisani na kufanya maombi.

Happygod Msuva amesema walifanya hivyo baada ya Msuva kulipwa Sh 200,000 na Moro United kama usajili wake.

“Baada ya kulipwa, tulichukua dau lote la usajili la Sh laki mbili alizokuwa amepewa. Tukaenda kanisani na kutoa sadaka yote, pia tutafanya maombi.

“Pamoja na juhudi kubwa anazofanya yeye pamoja na familia lakini tumekuwa tukifanya maombi, tunamuomba Mungu na kweli njia  tumekuwa tukiiona,” alisema.

Happygod ambaye ni fundi maarufu wa magari katika eneo la Mabibo, amesema anaamini mwanaye atapiga hatua zaidi kwa kuwa ni mtu anayetaka mafanikio.

Kwa sasa Msuva anakipiga katika kikosi cha Difaa Al Jadid cha Morocco.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV