August 19, 2017


Beki Marc Bartra ameifungia timu yake ya  Borussia Dortmund moja ya mabao matatu wakati ikiilaza Wolfsburg 3-0.
Bartra ambaye ni Mhispania aliyetokea Barcelona, alionyesha hisia zake kwa kubusu kitambaa cheusi kwa ajili ya maombolezo yanayotokana na shambulizi la kigaidi jijini Barcelona, juzi.

Kisoka, beki huyo amekulia katika chuo cha watoto cha Barcelona, maarufu kama La Masia.

Mabao mengi ya Dortmund dhidi ya Wolfsburg yalifungwa na Christian Pulisic na Pierre-Emerick Aubameyang.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic