Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameiahidi serikali mazuri kwa kutamka kuwa ubabaishaji basi kuanzia hivi sasa katika soka.
Kauli hiyo aliitoa dakika chache mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa ugombea wa urais wa shirikisho hilo akishindwa kwa kishindo, juzi Jumamosi kwenye Ukumbi wa St Gasper mkoani Dodoma.
Karia amesema soka la nchini limekuwa likishindwa kufanya mengi mazuri kutokana na ubabaishaji wa baadhi ya viongozi, hivyo hataki kuona hilo linatokea katika utawala wake ili kuhakikisha soka la nchini linapiga hatua.
Karia alisema hataiangusha serikali katika utendaji wake wa kazi huku akiomba ushirikiano kutoka kwao kupitia wizara ya michezo.
"Viongozi wote wapya tuna deni kubwa la kuwalipa Watanzania katika kuwapa mafanikio ya soka nchini. Kingine niwaahidi serikali kuwa sitawaangusha katika mafanikio ya soka, niwaambie ubabaishaji katika soka basi," alisema Karia.
0 COMMENTS:
Post a Comment