August 15, 2017


Baada ya zile taarifa kuwa Juuko Murshid anatarajia kutua Yanga, Simba wameamua kumshusha jijini Dar es Salaam.

Juuko raia wa Uganda ametua jijini Dar es Salaam na moja kwa moja amekwenda katika ofisi za mmoja wa wafadhili wa Simba, Mohammed Dewji.

Dewji maarufu kama Mo, ameonekana akiwa na Juuko pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

Kitendo cha Juuko kuonekana akiwa na Mo na Hans Poppe, imekuwa ni faraja kubwa kwa Wanasimba ambao wameanza kuwazodoa watani wao Yanga.

Hata hivyo, imeelezwa Juuko alikuwa na mpango wa kujiunga na Orlando Pirates ambayo itafunishwa na Sredojevic Milutin ‘Micho’ raia wa Serbia aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Uganda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic