Baada ya kumalizana na klabu ya Yanga kwa kusaini mkataba wa kujiunga nayo, kiungo Papy Kabamba Tshishimbi ataanza kuonekana uwanjani katika mechi dhidi ya Simba, wikiendi ijayo.
Tshishimbi raia wa DR Congo aliyekuwa akikipiga Mbabane Swallows ya Swaziland, amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.
Kiungo huyo mkabaji, amesajiliwa ili kuimarisha ukabaji na kuunganisha kiungo na ulinzi na hii ni baada ya kuondoka kwa Haruna Niyonzima.
Maana yake, Kocha George Lwandamina atamtumia kama kiungo mkabaji huku Thabani Kamusoko akiwa na nafasi ya kuichezesha timu.
0 COMMENTS:
Post a Comment