August 12, 2017Mabingwa wa Tanzania, Yanaga sasa wameweka wazi kuwa, wapo makini kuelekea dakika za mwisho za usajili wa wachezaji wa kigeni kwa kuhakikisha hawasajili magarasa kama ilivyotokea huko nyuma kwa mitego waliyokuwa wakiwekewa.

Usajili kwa wachezaji raia wa Tanzania umemalizika tangu Agosti 6, mwaka huu, lakini Yanga ina nafasi ya kusajili mchezaji mmoja wa kigeni hadi Agosti 15 ambapo usajili huo utafungwa.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema kipindi hiki wameamua kuwa makini zaidi ili kuepuka kusajili wachezaji wenye uwezo mdogo ambao huwaghalimu.

“Kuna wachezaji walikuja kwa ajili ya kufanya majaribio na tumeona hawana uwezo hao ni Mnigeria, Henry Okoh na Mcameroon, Ferdinand Bongyang ambaye tunamrudisha kwao muda wowote.

“Kwa sasa amebaki Yisa Mfowoshe ambaye ni Mnigeria huyu anaendelea kuangaliwa na tunasubiri majibu ya benchi la ufundi kama wameridhika naye ndiyo tujue mchakato wa kumsajili.

“Kumekuwa na tabia za mawakala kuleta wachezaji katika dakika za mwisho kwa ajili ya kufanya majaribio ambapo wamekuwa wakiangaliwa haraka haraka kisha wanasajiliwa.
“Huu ni mtego unaofanywa makusudi ili tuwasajili haraka bila kutathimini kwa kina uwezo wao, sasa tumeamua kuwa makini zaidi na suala hilo ili kusajili wachezaji wenye viwango na si vinginevyo,” alisema Mkwasa.

Wakati huohuo, kiungo mkabaji wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi anatarajiwa kuwasili nchini leo Jumamosi tayari kukitumikia kikosi hicho.

Tshishimbi raia wa DR Congo anawasili nchini baada ya Yanga kumalizana na klabu yake ya Mbabane Swallows ya Swaziland.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV