August 2, 2017




Kiungo rasta wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko juzi jioni alijiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo mkoani Morogoro na kuanza mazoezi muda huo na wenzake chini ya Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina.

Kamusoko alikuwa mchezaji pekee ambaye hakuwepo kambini, hivyo ujio wake umekamilisha idadi kamili ya wachezaji wa timu hiyo wanaojiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mzimbabwe huyo, hakuwepo kwenye kambi hiyo ya wiki mbili mkoani huko kwa ruhusa maalumu aliyoiomba siku moja tangu aongeze mkataba wa miaka miwili ya kubaki Yanga. Aliomba ruhusa ili arudi nyumbani kwao kwa ajili ya kutatua matatizo ya kifamilia.

 Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema Kamusoko mara baada ya kuripoti kambini jioni alianza mazoezi ya pamoja na wenzake huku akifanya programu zote kwa usahihi.

Saleh alisema, kiungo huyo alifanya programu zote ikiwemo ngumu na nyepesi na yeye mwenyewe aliomba kwani akiwa kwao alikuwa akifanya mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti.

Aliongeza kuwa, kambi hiyo inaendelea vizuri na wachezaji wote wapo fiti na anafurahia kumuona beki wa pembeni, Hassan Kessy akirejea uwanjani akitoka kwenye majeraha ya nyama za paja aliyoyapata akiwa timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa inashiriki michuano ya Cosafa, Sauzi.

"Kambi yetu Morogoro inaendelea vizuri na niseme kuwa vijana wana hari na morali ya hali juu kwa ajili ya kuanza ligi kuu na wachezaji wetu tayari wameripoti kambini.

"Na leo (jana) jioni Kamusoko aliripoti kambini Morogoro na alianza mazoezi ya pamoja na wenzake muda mchache tangu ajiunge na wenzake, hivyo niseme kikosi chetu kimekamilika.

"Kuhusu majeruhi hakuna hadi hivi sasa, Kessy aliyekuwa na majeraha ya nyama za paja aliyotoka nayo timu ya taifa yamepona na yupo fiti," alisema Saleh.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic