August 23, 2017




Muda mfupi kabla ya mchezo wa Yanga dhidi ya Simba kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwania Ngao ya Jamii, mshambuliaji wa zamani wa Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni amezungumzia mchezo huo.

Kibadeni amesema anaamini katika mchezo huo rekodi yake ya kufunga mabao matatu  ‘hat trick’ katika mchezo baina ya Simba na Yanga, itafunzwa pale kwenye Uwanja wa Taifa.

Mkongwe huyo ambaye kwa sasa ni kocha amesisitiza kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi na kudai kuwa hata Yanga wenyewe wanajua kuwa lazima wafungwe katika kipute hicho kitakachoanza saa 11:00 jioni ya leo.

“Rekodi yangu itavunjwa leo pale Taifa, na atakayevunja ni mchezaji wa Simba kwa kuwa kuna wachezaji wazuri,” alisema Kibadeni.

Kuhusu Ibrahim Ajibu na Haruna Niyonzima alisema: “Niyonzima ndiye ambaye atawamaliza, si unaona hata Yanga wenyewe walikuwa wakimlilia, Ajibu hakutakiwa na Simba ndiyo maana akaachiwa akaondoka, wangekuwa wanamtaka wasingemruhusu aondoke kirahisi.”

Rekodi ya Kibadeni ya kufunga hat trick haijavunjwa kwa miaka 40 sasa, kwani aliiweka Julai 19, 1977 ambapo Simba iliifunga Yanga mabao 6-0 na kuweka rekodi ya kuwa kipigo kikali zaidi baina ya timu hizo kuwahi kutokea.


Katika mchezo huo Kibadeni alifunga mabao hayo katika dakika ya 10, 42 na 89, mengine yalifungwa na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60 na 73 huku lingine likiwekwa wavuni na Selemani Sanga dakika ya 20 baada ya kujifunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic