August 19, 2017



Unaweza kusema ilikuwa hali ya kushangaza mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wa Simba na Yanga ilibaki kidogo wachapane makonde baada ya mmoja wao kumsema vibaya beki kitasa wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Ninja amekuwa maarufu kutokana na staili yake ya kucheza pia kusababisha penalti katika mchezo dhidi ya Singida United kabla ya kujifunga bao dhidi ya Ruvu Shooting.

Tukio la mashabiki hao kutaka kupigana lilitokea juzi katika eneo la Jang’ombe Gengeni jirani na ilipo Klabu ya Taifa Jang’ombe aliyotokea Ninja kabla ya kusajiliwa na Yanga hivi karibuni.

Kama utani, shabiki wa Yanga aitwaye Hassan Ameir alianza kutoa maoni yake kwa gazeti hili kuhusu beki huyo na alipolitaja jina la Ninja tu, akaibuka shabiki mwingine aliyedaiwa kuwa wa Simba na kuanza kumponda beki huyo.

Kitendo hicho kilisababisha zogo kubwa kwa wawili hao huku kila mmoja akitetea upande wake kiasi cha baadhi ya wapita njia kuwashangaa.

Ameir alisikika akisema: “Nimeanza kuipenda Yanga kwa sababu ya Ninja, sasa wewe unaniambia kitu gani ambacho nitaweza kukuelewa, endelea kuipenda Simba na Azam yako kwa sababu jamaa yako anacheza pale.”

Kuona hivyo, yule shabiki wa Simba naye akajibu mapigo ndipo walipovaana kabla ya kuamuliwa na watu waliokuwepo eneo hilo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic