August 19, 2017



Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba raia wa Romania amesema atatumia mikanda ya video kuangalia mechi zao zote za kirafiki ili kufuta makosa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.

Miongoni mwa timu 15 atakazopambana nazo Cioaba ni Simba, Yanga, Singida United, Mbeya City na Mbao FC.

Azam ambayo mwanzoni mwa wiki hii ilitua jijini Dar es Salaam ikitokea Uganda ilipoweka kambi ya muda mfupi kujiandaa na msimu ujao, ikiwa huko ilicheza mechi tano za kirafiki bila ya kupoteza.

“Nimerejea kumalizia maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza ligi kwa kucheza na Ndanda, nina DVD (mikanda ya video) za mechi zetu zote za kirafiki nikijaribu kukaa na wenzangu ili kuchambua wapi kulikuwa na makosa ili tuyafanyie kazi.

“Tunataka ligi ikianza kila kitu kiwe sawa yaani yale makosa madogomadogo yaliyobakia yasiwepo ili tuwe tunapata matokeo mazuri tu kila tunaposhuka uwanjani,” alisema Cioaba.

Katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Agosti 26, mwaka huu, Azam itacheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo Mtwara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic