August 3, 2017


Neymar ameweka rekodi mpya ya usajili baada ya kumalizana na PSG ya Ufaransa kwa day la pauni million 198.

Neymar raia wa Brazil amesaini mkataba huo na Paris Saint-Germain ya Ufaransa na sasa atakuwa akipokea mshahara wa pauni 500,000 na kuwa mchezaji ghali zaidi kwa kipato duniani.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 25, ameondoka Barcelona huku wengi wakiwa hawajatarajia.


Tayari jezi namba 10 imetangazwa kuwa yake na kesho mchana atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wa PSG kwenye Uwanja wa Parc des Princes jijini Paris.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV