August 20, 2017



Kocha wa Yanga, George Lwandamina amewataka wachezaji wake kuelekeza nguvu katika maandalizi ya kutosha kwa kuwa hakutakuwa na maandalizi ya mwanzo wa msimu tena baada ya hapo.
Yanga iko kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Jumatano.

Lakini Lwandamina raia wa Zambia amekuwa akisisitiza kwamba, maandalizi yao ni kwa ajili ya msimu wot.

“Unajua baada ya hapo, hakuna pre season. Kocha amewaambia wachezaji ni lazima kujiandaa kwa uhakika.

“Amewaambia baad ya maandalizi hayo itakuwa ni maandalizi madogo na vizuri kila mmoja akautumia muda huu vizuri,” kilieleza chanzo.


Aidha, Lwandamina amewataka wachezaji kuamini, kila mechi inayokuwa mbele yao, wahakikishe wanafanya vizuri kwa uchezaji kila mmoja katika nafasi yake ili kuifanya timu yao iwe bora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic