August 3, 2017


Mashabiki wa Barcelona, nao wameonyesha wan a tabia za ‘kiting’ baada ya kuchoma jezi namba 11 ambayo ilikuwa ikivaliwa na mshambuliaji Neymar dos Santos.

Neymar yuko katika hatua ya mwisho kujiunga na PSG ya Ufaransa, mambo ambalo linaonekana kuwaudhi mashabiki hao.

Wiki kadhaa zilizopita mashabiki wa Yanga, nao walifanya kitendo hicho kinachoonyesha kukiuka uanamichezo wenye urafiki kwa kucheza jezi ya Haruna Niyonzima aliyeondoka Jangwani na kujiunga na Simba.

Video ya mashabiki waliochoma jezi hiyo ya Neymar imekuwa ikisambaa mitandaoni ingawa inashindwa kujulikana ni mashabiki wa wapi.


Mashabiki hao wamekuwa wakilalamikia usaliti katakana na kitendo cha Neymar kuamua kuondoka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV