August 4, 2017Mwamuzi anayetarajia kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii anatarajia kupangwa leo Ijumaa na kamati ya waamuzi iliyo chini ya Salum Chama.

Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga inatarajia kuchezwa Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ikiwa ni utambulisho wa msimu mpya wa ligi kuu inayotarajia kuanza Agosti 26.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Chama alisema kamati yao inatarajia kukutana leo kwa ajili ya kupanga ratiba ya waamuzi watakaochezesha ligi msimu ujao wa ligi kuu ikiwa na mchezo wa Ngao ya Jamii na kudai kuwa mwamuzi atakayechezesha mchezo huo lazima awe na ubora.


“Tunatarajia kupanga ratiba ya waamuzi siku ya Ijumaa kulingana na wale ambao wamefaulu katika mtihani wa copa test,” alisema Chama. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV