Mwenyekiti wa Yanga Tawi la Kitunda jijini Dar es Salaam, Boaz Ikupilika anawakaribisha wanafanya katika sherehe ya ubingwa wa 27 ukiwa pia ni wa mara ya tatu mfulilizo.
Kombe hilo la ubingwa wa Tanzania Bara tutalitembeza Kesho Jumapili mitaa ya Ukonga na baadaye litafika tawini na pia wanachama wapya watapata fursa ya kujisajili na benki ya posta na kukabidhiwa kadi zao.
Sherehe zitaanzia tawi la Majumbasita kuanzia Saa 3:00 asubuhi na kupitia mitaa ya Ukonga na kurudi njia ya banana mpaka kitunda na mitaa yake
Baadaye litarejea Majumbasita ambapo sherehe zitapambwa na burudani ya Msaga Sumu na shamrashamra nyingine kibao.
Karibuni sana.
Mimi mwenyekiti wa Tawi.
0 COMMENTS:
Post a Comment