August 12, 2017


MGOMBEA wa nafasi ya Ujumbe ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Mazengo kutoka Kanda ya sita (Katavi na Rukwa, amejikuta akishindwa kujibu swali alipopewa nafasi ya kuomba kura.

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika leo mjini hapa kwenye Ukumbi wa St Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Ilikuwa hivi; Muda wa wagombea kuomba kura kwa mara ya mwisho ulipofika, mgombea Mazembe alipanda jukwaani na kuelezea mikakati yake na alipomaliza mjumbe mmoja akanyosha mkono na kumtaka ataje vyama vya soka vinne vinavyounda Kanda ya Katavi lakini akashindwa na kuibua minong’ono kwa wajumbe wengine.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV