August 1, 2017

PICHA MFANO NIYONZIMA ATAKAVYOKUWA AKIONEKANA KATIKA UZI WA SIMBA.


Leo au kesho, kiungo Haruna Niyonzima anaweza kuungana na wenzake Afrika Kusini.

Sasa una sababu ya kuwa na hofu kwa kuwa Simba wenyewe wameshasema Niyonzima ni mchezaji wao.


Awali kulikuwa na uficho wa mambo, lakini sasa kila kitu kiko hadharani kuwa Niyonzima atavaa jezi nyekundu na nyeupe msimu wa 2017-18.

Simba waliendelea kufanya siri usajili wa Niyonzima kwa kuwa mkataba wake na Yanga wakati wakimalizana naye haukuwa umekamilika.

Lakini sasa Simba wamevunja ukimya na wanaweza kulizungumzia suala hilo hadharani kwa kuwa mkataba wa Yanga na kiungo huyo Mnyarwanda umekamilika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV