August 26, 2017



FULL TIME
Dk ya 92: Mchezo umemalizika, Simba wamepata ushindi mnono wa mabao 7-0.
Dk ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Dk ya 89: Kiungo wa Simba Kotei anachezewa faulo, amchezo unasimama kwa muda.
Dk ya 85: Simba wanaongoza kwa mabao saba hadi sasa, Ruvu wanatumia muda mwingi kulaumiana.
Simba wanapata bao la saba kutpia kwa Erasto Nyoni.
Dk ya 82: GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 80: Wachezaji wa Simba sasa wanaonyesha ufundi uwanjani.
Dk ya 75: Mchezo ni wa kushambuliana kwa zamu.
Dk ya 70: Kasi ya Juuko bado haijachanganya.
Dk ya 65: Simba wanafanya mabadiliko, wanamtoa Mwanjali, anaingia Juuko. 
Dk ya 61: Kichuya anapata nafasi ya kufunga lakini anakuwa ameotea. 
Dk ya 57; Mchezo unaendelea kwa kasi, Simba ni kama hawajatosheka na mabao waliyofunga.
Dk ya 51: Okwi anaipatia Simba bao la Sita, anafunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Saidi Ndemla ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Niyonzima aliyeumia.
Dk ya 51: GOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 50: Ruvu wanasogea kwenye lango la Ruvu lakini wanazuiwa.
Dk ya 48: Simba wanacheza mchezo wa nguvu, Kotei anacheza faulo katikati ya uwanja.Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Dk ya 47: Mwamuzi anamaliza kipindi cha kwanza Simba wakiwa mbele kwa mabao 5-0.
Simba wanapata bao la tano likifungwa na Juma Liuzio akimalizia krosi nzuri ya Nyoni.
Dk ya 46: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Simba wanapata bao la nne kupitia kwa Kichuya, alipata krosi nzuri kutoka kwa Nyoni akamalizia kiulaini.
Dk ya 42: GOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 40: Mashabiki wa Simba wanashangilia kwa nguvu hapa kwenye Uwanja wa Uhuru.
Dk ya 38: Simba wamemiliki mchezo kwa muda mrefu sasa.
Pasi nzuri kutoka kwa Mzamiru, inatua mguuni kwa Okwi, akiwa yeye na kipa anatupia bao la tatu.
Okwi tenaaaaaaaaa
Dk ya 35: GOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!
Dk ya 32 Mchezo unaendelea, Manula ameshatibiwa.
Dk ya 30: Mchezo umesimama, kipa wa Simba, Aishi Manula amelala chini baada ya kuumia.
Dk ya 25: Simba wanamiliki mpira muda mwingi, mashabiki wao wanashangilia kwa nguvu.
Okwi tena anaipatia bao la pili Simba, amewapiga chenga mabeki wawili na kutupia mpira wavuni.
Dk ya 22: Gooooooooooooooooooooo!
Dk ya 20: Simba wanaongoza bao 1-0.
Okwi anaipatia Simba bao la kwanza baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Ruvu kisha kupiga shuti lililojaa wavuni moja kwa moja, alipata pasi kutoka kwa Mzamiru.
Dk ya 18: Okwiiiiiiiiiiiiiiii
GOOOOOOOOOOOOOOOOO!!
Dk ya 16: Ruvu wanacheza vizuri kadiri muda unavyokwenda, wanapa upinzani Simba.
Dk ya 14: Mzamiru anacheza faulo katikati ya uwanja, unapigwa mpira kuelekea kwa Simba.
Dk ya 10: Simba ndiyo ambao wamefila langoni mwa Ruvu lakini hawajaweza kutengeneza mashambulizi ya nguvu.
Dk ya 6: Simba wanalishambulia lango la Ruvu lakini bado kasi haijachanganya.Dakika ya 1: Timu zote zimeanza kwa kasi ndogo.
Mchezo umeanza.
Timu zimeshaingia uwanjani.

SIMBA SC 
1. Aishi Manula-28
2. Ally Shomary-21
3. Erasto Nyoni-18
4. Method Mwanjale-17
5. Salum Mbonde-2
6. James Kotei-3
7. Shiza Kichuya-25
8. Mzamiru Yassin-19
9. Juma Liuzio-10
10. Emmanuel Okwi-7
11. Haruna Niyonzima-8

SUB
1. Emmanuel Mseja-30
2. Jonas Mkudeh-20
3. Mohamed Ibrahim-4
4. Said Ndemla-13
5. Laudit Mavugo-11
6. Juuko Murshid-6
7. Mohamed Hussein-15

Kocha... 
MARIUS OMOG

RUVU SHOOTING. 

1. Bidii Hussein-18
2. Said Imani Madega-19
3. Yusuph Innocent-2
4. Shaibu Nayopa-26
5. Mangasin Mangasin-6
6. Baraka Mtuwi-15
7. Chande Magoja-21
8. Shaban Msaja-4
9. Juma Said-9
10. Jamal Mtegeta-10
11. Khamis Mussa-22

Subs. 

1. Abdallah Rashid-1
2. George Wawa-12
3. Mau Ally-23
4. Frank Msese-16
5. Kassim Dabi-24
6. William Patrick-27
7. Said Dilunga-25

Kocha.. 
ABDUL MUTIK HAJI

Kick Off-16:00

Venue: Uhuru Stadium.
KUNJI/C

1 COMMENTS:

  1. Duh Ruvu shooting vipeee.....tano bila kipindi cha kwanza??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic