August 25, 2017



Na Joseph Msami, New York 
Maisha yamerejea katika hali ya kawaida baada ya homa ya pambano la Ngao ya Jamii la watani wa jadi Simba na Yanga kuhitimishwa Jumatanio katika uwanja wa taifa,   kwa ushindi wa penalti ambapo Simba walipata mikwaju mitano dhidi ya minne ya Yanga.

Kwamba Simba ni bingwa hilo halina ubishi, historia imeandikwa na sasa kinachosubiriwa ni kuanza kwa msimu wa ligi kuu ambapo timu hizo zitakutana tena.

Kwa sababu ya tofauti ya muda huku ughaibuni ( Marekani) na bongo, wakati mpambano unaendeleaa nilikuwa kazini, nilijitahidi kufuatilia japo sio kwa uhuru ambao nilitamani kuwa nao. Nilitumia kipatakalishi ( Kompyuta) yangu ya kazi kufanya kila ambacho waweza kukiita kupiga chabo, huku majukumu mengne yakitakiwa kuendelea.

Kabla ya mchezo kuanza nilimtumia rafiki yangu David Gile ujumbe ambao ninaunukuu hapa ‘Hizi timu zimetumia muda mwingi sana kucheza nje ya uwanja hasa Simba. Ngoja sasa tuone uwanjani itakuwaje, Kila la heri.’’ David ambaye nimsahabiki wa Simab hakunielewa na 

Nilichokuwa najaribu kumweleza hapo ni jinsi gani Simba ambavyo wameucheza mpira nje ya uwanja. Japo hakunielewa kwakuwa alidhani naikashifu timu yake , lakini nilimaanisha kile ambacho natamani wanamichezo leo wakifahamu.

Tangu usajili na kuelekea pambano hilo Simba walionekana wazi kujimanini kwamba wataifunga Yanga na ndicho kiichotokea. Labda ni kwa kuwa wamefanya usajili wa zaidi ya shilingi bilioni moja na wamesajili wachezaji wazoefu ikilinganishwa na misimu michache iliyopita ambapo walikuwa na makinda wengi.

Mashabiki waliongeza nguvu Simba
Mashabiki wa Simba walijiandaa kisaikolojia kushinda hatua iliyoambukiza akili za wachezaji ambao walionekana wamedhamiria zaidi. Hata takwimu za mchezo zinaionsb ahilo.  Mara kadhaa uwanjani mashabiki wa Simba walionekana wenye msisimko mkubwa ikilinganishwa na wale wa Yanga, na kama wataalamu wa soka wasemavyo, mashabiki huchochea ushindi ndicho kilichotokea.

Hata baada ya dakika 90 kumalizika, morali ya wachezaji hao ilikuwa juu, na walipoanza kupiga penalti pia mashabiki wako walianikiza kwa kasi ushindi wao. Wakati Kelvini Yondani anaenda kupiga penalti ya kwanza kwa Yanga, mtangazaji wa kituo nilichokuwa nashuhudia alisema ‘‘Yanga leo wamepooza’’ Maneno hayo ni kama vile Yondani aliyasikia. Au pia labda aliona unyonge wa washabiki wake akakosa kujiamini. ( Hizi ni hisia zangu).

Usiri wa Yanga
Yanga wamekuwa wakitumia mbinu ya kuwa kimya, kutoeleza kuhusu kambi, wakiamini kuwa sio lazima kupiga kelele nje ya uwanja. Ni kweli kwamba wakati fulani mbinu hiyo ilionekana kuwa bora kwani walivyoibuka kutoka Pemba walishinda mchezo wao wa ligi  ambao Simba waliutawala pia nje ya uwanja na kuonekana kama wangeshinda. 

Hata wachambuzi waliipa nafasi kubwa Simba. Mbinu hii yaweza kuwa bora lakini wakati huu pengine ukiongeza na matatizo ya ukata wa fedha unaokabili wana Jangwani hao, mbinu haikufanya kazi. Nafikiri viongozi wasome alama za nyakati.


Wachezaji wa Simba wawashukuru mashabiki
Wakihojiwa baada ya mchezo, wachezaji Haruna Niyonzima na Emanuel Okwi,wamewashukuru mashabiki wao kwa kuonyesha mshikamano wa hali ya juu kabla na wakati wa mchezo. Wachezaji hawa wa kimataiafa na amabo wanajua matarajio waliyonayo wekundu wa msimbazi kwao, wanaweka bayana kuwa mchango wa mashabiki ni muhimu katika ushindi. 

Hili linadhihirisha wazi niliyotangulia kusema kuwa Simba waliandaliwa kisaikolojia na wakaongezewa nguvu na hamasa ya mashabiki lakini mashabiki wa vijana wa Jangwani, Yanga, walionekana kuwa wanyonge wakitishiwa na mkwala wa wapinzani wao.

Okwi alithubutu kusema kuwa hawakutegemea ushindani mkubwa kama huo. Hii inamaanisha waliingia kushind aidadi nyingi ya magoli ndiyo mana walicheza attacking game. Wapinzani wao walitumia muda mwingi kulinda lango licha ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza. 

Mitandao ya kijamii
Ni kawaida watani hawa wa jadi kurushiana vijembe ,kabla, wakati na baada ya mpambano. Nilijaribu kurambaza makundi mengi ya Watsup ambapo pia niliona wazi kuwa mashabiki wa Simba waliwahadaa wenzao wa Yanga kuwa safari hii wanawaua tena kwa idadi kubwa ya magoli.

 Ilionekana mzaha, lakini mara nyingi huumba jambo. Mbwembwe zao zilinogeshwa na msemaji wa klabu Haji Manara ambaye video yake akijigamba kuwa watatoa kipigo cha msimu ilikoleza moto. 


Kushangilia kwa matukio
Utamaduni wa nchi yetu (na nchi nyingi Afrika) ni kushangilia kwa matukio. Hili ni tofauti sana na wenzetu mathalani nchi za Ulaya ambapo hushangilia muda wote. Katika mchezo wa Jumatano, Yanga waliendeleza mtindo huo. Hali ilikuwa tofauti kidogo kwa Simba ambao muda mwingi walishangilia na kuipa hamasa timu. 

Mathalani wakati wa upigaji wa penalti, Simba walishangia wakati wapigaji wa timu yao wakienda kupiga. Mashabiki wa Yanga waliibuka kwa msimu hasa pale Mohamed Hussien Zimbwe maarufu kama Tshabalala alipokosa mkwaju wa penalti.

Wataalamu wa soka wanasema mchezo wa mpira wa miguu unaanzia nje,  kisha ndani ya uwanja wakimaanisha mashabiki wana asilimia kubwa ya ushindi wakiiunga mkono timu yao. Yanga na Simba zina vikosi vizuri na kwa mchezo wa jusi timu hizi zikikaa kwa pamoja muda mrefu mchezo wa ligi utakuwa wa kusisimua zaidi na lolote laweza kutokea. 

Joseph Msami Msami ni mwanamichezo aishie Marekani kikazi kwa sasa, ikiwa una maoni unaweza kumuandikia katika namba hii inayopatikana pia kwa Watsup +1 646 546 4122




2 COMMENTS:

  1. Heko mwandishi kwa kubainisha kwamba saikolojia inasaidia sana kuongeza confidence kwa wachezaji ikiwa wataaminiwa.Mourihno alipohojiwa baada ya mechi na Swansea alisema confidence ya wachezaji wake imechangia kushinda.Ukiingia kinyonge unacheza kinyonge. Mashabiki unaambiwa ni mchezaji wa 12.Hiyo ndio waandishi wa michezo Bongo wakisikia mashabiki wakitamba wanafasiri kwamba timu imesajili malaika hivyo haifungwi. Kumbe ukweli ni kwamba timu karibu zote kubwa zina wataalamu wa saikolojia kuwajenga wachezaji wajiamini.

    ReplyDelete
  2. Washabiki wa Yanga ni washangiliaji wazuri lkn kwa sasa kinachowapa unyonge ni Niyonzima kuhamia Simba.
    Nakumbuka kipindi kile Luis Figo akiondoka Barcelona na kutimkia Real Madrid iliwasonenesha sana na kwa muda mrefu mashabiki wa Barcelona walikuwa wanyonge na mbaya zaidi Figo aliunganisha majeshi na Zinadine Zidani ikawa moto na kuwapagawisha mashabiki wao wa Real Madrid.
    Mashabiki wa Simba nayo walikuwa na wakati mgumu kipindi cha miaka mitatu ya nyuma wakati kina Yondani, Barthez, Okwi, Kessy walivyochezea Yanga na mashabiki wengi wa Simba walikuwa hawaendi uwanjani kushangilia timu yao na kuna kipindi nakumbuka Hans Pope na Haji Manara walikuwa wanawahimiza mashabiki kwenda uwanjani kwani mashabiki anapohudhuria mechi anahesabika ni mchezaji no.12.Kweli kama ulivyotuhabarisha ushangiliaji kwa timu ni moja ya hamasa kubwa kwa wachezaji na kumbuka enzi za kocha Maximo na alivyokuwa anahamasisha mashabiki kuishangilia timu ya taifa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic