August 25, 2017



Uongozi wa Simba umewapa kifuta jasho wachezaji wake baada ya juzi Jumatano kufanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Mchezo huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Simba kupata ushindi wa penalti 5-4 baada ya matokeo ya suluhu katika dakika 90.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kwamba kabla ya mechi hiyo uongozi wa Simba uliwaahidi kuwapatia wachezaji hao kitita hicho kama wataifunga Yanga.

“Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuibuka na ushindi katika mchezo huo lakini pia kwa kazi kubwa iliyofanywa uwanjani na wachezaji wetu.

“Hata hivyo, kabla ya mechi, tuliahidi kuwa endapo wataifunga Yanga basi tutawapatia kifuta jasho cha shilingi milioni 40 kwa hiyo Mungu akipenda siku yoyote kuanzia sasa tutawapatia fedha zao hizo.

“Fedha hizo zitatolewa na uongozi lakini pia ile bonasi Sh milioni 10 ambayo msimu uliopita walikuwa wakipewa kutoka kwa wanachama wetu kila walipokuwa wakishinda nayo watapewa,” kilisema chanzo hicho cha habari.


Alipoulizwa kuhusiana na hilo Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara hakuwa tayari kusema chochote zaidi ya kudai kuwa suala hilo ni la ndani ya timu kwa hiyo hawezi kusema chochote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic