August 9, 2017
Kocha wa Makipa wa Simba, Mwarami Mohammed ‘Shilton’, amesema Aishi Manula na Said Mohammed ‘Nduda’ ni aina ya walinda mlango wanaotakiwa hasa kuitumikia timu hiyo kutokana na uzoefu waliokuwa nao kwenye michuano mbalimbali.

Kocha huyo ameyasema hayo ikiwa Manula aliyejiunga na Simba akitokea Azam na Nduda akitokea Mtibwa Sugar, wakiwa wamepewa mikataba ya miaka miwili kila mmoja, wakionekana kuwa na vita ya namba kwenye kikosi hicho.

Shilton alisema, timu kama Simba ambayo itakuwa na mashindano mengi, inatakiwa kuwa na wachezaji wazoefu na wenye uwezo wa hali ya juu katika idara zote ikiwemo golini.

“Vita ya namba baina yao itakuwepo tena si ndogo, lakini hii ndiyo inatakiwa kuonekana kwenye timu yoyote ile inayotaka kuwa na ushindani.


“Ukiangalia Simba itashiriki michuano ya ligi kuu, Kombe la FA pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo inakupasa kuwa na makipa kama hawa, kwangu najisikia furaha kuwa nao wote, kazi iliyobaki kwao ni kudhihirisha uwezo wao.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV