August 9, 2017Kampuni ya SportPesa imezindua rasmi promosheni ya mtambulishe rafiki ijulikanayo kama Rafiki Bonus ambapo mtambulishaji atajipatia TZS 2000/- kama bonus ya utambulishaji huo.

Mteja wa SportPesa ambaye tayari amekwisha jisajili na kuanza kucheza, anachotakiwa kufanya ni kumtambulisha rafiki yake ambaye akijisajili na akianza kucheza, mteja aliyemtambulisha atapata hiyo bonus ya TZS 2000/-.

“Kampuni imekuja na Bonus ya Rafiki ikiwa kama njia ya kurudisha fadhila kwa wateja wetu. Tunawafurahia wateja wetu, na tunajua kuwa wamekuwa wakiwafundisha rafiki zao namna ya kubashiri na SportPesa. Hivyo basi, tumeona ni vyema na sisi tuwawekee mazingira ya wao kunufaika kwa uaminifu wao na Kampuni.

 Bonus ya Rafiki inamuwezesha mteja kupata elfu mbili (TZS 2000/-) kwa kila mteja anayemtambulisha katika jukwaa la kubashiri na SportPesa.” Pavel Slavkov, Mkurugenzi Mkuu SportPesa. 

Ili mteja aweze kufuzu kushiriki katika bonasi ya Rafiki; mteja anatakiwa awe amejisajili na awe mtumiaji wa SportPesa kubashiri. Pia, mteja mpya ambaye anatambulishwa na rafiki yake, anatakiwa kutuma neno KUBALI kisha kuandika namba ya simu ya mtu aliyemkaribisha katika jukwaa la kubashiri la SportPesa, mfano KUBALI 0700XXXXXX. Mteja mpya atatakiwa kuweka ubashiri angalau mara moja katika michezo ya Jackpot, kwenye mchanganyiko wowote wa Multi Bet bila kujali aina ya mchezo, au kuweka Single Bet kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu yenye soko la njia tatu (1,X,2) - yaani ushindi wa nyumbani (1), suluhu (x) au ushindi wa ugenini (2) ambapo odds za soko atalochagua ziwe zaidi ya 1.60.  
Mteja anaweza kubashiri kwa njia ya ujumbe (SMS) au kwa njia ya tovuti (www.sportpesa.co.tz) ambapo atafuata hatua zilizo elekezwa ili kushiriki kwenye bonus hiyo.
Uzinduzi wa Rafiki Bonus ni sehemu moja wapo ya Kampuni ya SportPesa katika kuwaburudisha wateja wake ambao, kwa kipindi kirefu sasa tangu Kampuni kuanza shughuli zake nchini, wamejisajili kikamilifu na wengi wao wamesaidia rafiki, ndugu na jamaa kujiunga na kubashiri kutumia majukwaa ya Sportpesa. 

SportPesa inajivunia kuwa na kiasi kikubwa cha pesa ya Jackpot kwa sasa cha fedha za Kitanzania milioni mia mbili na tatu (TZS 203,391,920), odds zinazovutia na huduma kwa wateja yenye daraja la kimataifa iliyopo hewani masaa 24 kuwafikia wateja waliopo na wateja wapya wanaopenda kujua zaidi kuhusu huduma za kampuni.  Wateja wanashauriwa kupiga simu za huduma kwa wateja 0764115588, 0658115588 na 0692115588 kwa taarifa zaidi kuhusu bonasi ya rafiki. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV