August 9, 2017Mgombea wa Urais wa TFF, Frederick Mwakalebela amesema ataufanya mpira kuwa biashara ya vijana.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mwakalebela amesema, mpira utakuwa biashara inayozaa kubwa kwa vijana.

Kama hiyo haitoshi, Mwakalebeba amesema ataboresha miundombinu mbalimbali.

“Lazima tuwe na miundo mbinu bora kama unataka kucheza soka. Sisi tunaona mambo yetu hayako vizuri na tunajua hali ya viwanja vyetu. Hili ni kati ya jambo nitakalolifanyia kazi.

“Nimesikia sera kadhaa, watu wanazungumza mambo ya kufikirika. Lakini mimi nilijipima nikiwa katibu mkuu wakati wa Tenga. Najua nini cha kufanya ili mambo yaende na kuzaa mafanikio,” alisema.
Uchaguzi Mkuu wa TFF umepangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV