August 15, 2017




Huenda ukawa umesikia au kuona kuhusu promosheni ya RAFIKI BONUS kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa na ukawa umeshajiuliza sana kuhusiana na promosheni hii na jinsi inavyofanya kazi, lakini mwisho wa siku ukaishia kukosa majibu sahihi au majibu uliyopata hayakukidhi haja yako.

Hakuna haja ya kuumiza kichwa tena kwani Makala hii ina lengo la kukuelewesha hatua kwa hatua kuhusiana na promosheni na RAFIKI BONUS hivyo twende sambamba.

Rafiki Bonus ni nini?
Rafiki Bonus ni promosheni kutoka kampuni ya SportPesa ambayo ina lengo la kukuzawadia Shilingi 2000/= za kitanzania wewe mteja wa SportPesa kwa kila rafiki yako unayemualika kujisajili na kucheza na SportPesa.

Hii ni sawa sawa na kusema kuwa kwa kila rafiki unayemualika kujisajili na SportPesa halafu rafiki yako huyo akaweka ubashiri wake basi wewe uliyemualika utakuwa umejipatia Sh 2000/=, hivyo kwa mahesabu ya haraka haraka kuwa kama ukiweza kualika marafiki 10 kwa siku moja wakajiunga na kuweka ubashiri wao utakuwa ina maana utakuwa umepata Sh 20,000/=

Sasa umeshajua Rafiki Bonus ni nini hivyo bila shaka utakuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua jinsi ya kumualika rafiki yako ili uweze kujivutia mkwanja huo. Wala usiwe na haraka, twende sambamba.

Jinsi ya Kumualika rafiki
Kama wewe ni mteja wa SportPesa ambaye unaweka utabiri wako mara kwa mara angalau mara moja ndani ya mwezi mmoja basi ni rahisi sana kwako kwasababu unachotakiwa kuanza kufanya ni kumshawishi rafiki yako kujisajili na akikubali kufanya hivyo basi unachotakiwa kufanya ni:

  1. 1. Hakikisha rafiki yako anajisajili na kuwa mteja wa SportPesa kama ulivyo wewe kwa kuingia kwenye uwanja wake wa SMS na kutuma neno RAFIKI kwenda 15888 ambapo atatumiwa ujumbe mfupi kutoka SportPesa utakaomtaka atume neno KUBALI likifuatiwa na namba yako wewe ya simu kwenda 15888
(Mfano: KUBALI 07XXXXXXXX kwenda 15888) huku pia akitakiwa kubofya link ya sportpesa.co.tz ili kusoma vigezo na masharti


ANZA HIVI...

HALAFU...
 








au kwa kubofya Sportpesa.co.tz/join na kisha aweka namba yako ya simu uliyojisajilia SportPesa kwenye kiboksi cha juu kulia wakati akiwa anajisajili


  1. 2. Baada ya kujisajili rafiki yako huyo atatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti yake kupitia M-Pesa kwa wateja wa Vodacom na Airtel Money kwa wateja wa Airtel kupitia namba ya kampuni ambayo ni 150888 kwa mitandao yote hiyo miwili.

  1. 3. Baada ya kuweka salio kwenye akaunti yake, basi rafiki yako huyo atatakiwa kubashiri kwenye masoko ya 

  • Michezo ya Jackpot au 
  • Multibet bila kujali aina ya mchezo au 
  • Single bet kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu yenye soko la njia tatu (I,X,2) yaani ushindi nyumbani (1), suluhu (X), au ushindi wa ugenini (2) ambapo odds za soko atakalochagua ziwe zaidi ya 1.60

Hakikisha rafiki yako huyo anajisajili na kuweka ubashiri kwani akijisajili pekee bila kuweka ubashiri haikufanyi wewe kushinda hadi pale atakapofanya vyote kwa pamoja.


Nifanyeje kama mimi sio mteja wa SportPesa?
Kama wewe sio mteja wa SportPesa bado unaweza kuwa sehemu ya RAFIKI BONUS endapo kama utajisajili kwanza ili uweze kuwa mteja wa SportPesa kwa:

Kutuma GAME kwenda 15888 au kwa kubofya sportpesa.co.tz/join kisha ufuate maelekezo.


Ukishajisajili sasa utatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti yako kupitia M-Pesa au Airtel Money ambapo namba ya kampuni ni 15888 kwa mitandao yote.


Utatakiwa kuweka ubashiri wako ili uweze kukidhi vigezo vya kumualika rafiki yako kupitia RAFIKI BONUS.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic