August 4, 2017Yanga imeamua rasmi kuachana na kiungo wake, Justine Zulu.

Uongozi wa Yanga kupitia katibu wake Mkuu, Charles Boniface Mkwasa umesema umeshafanya mazungumzo na mhusika anayemwakilisha Zulu na wamekubaliana kuvunja mkataba kwa siku zilizobaki.

“Tumekubaliana na sasa tutavunja mkataba kupitia makubaliano hayo,” alisema Mkwasa.


Awali, Zulu alitishia kuishitaki Yanga Fifa kwa madai ana mkataba lakini imekuwa ikimzungusha na hakujua hatma yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV