September 22, 2017


Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ameahidi kupata ushindi katika mechi ya kesho huku akitamba ni lazima wazichukue pointi tatu. 

Nsajigwa alisema, maandalizi ya macho yamekamilika ya mchezo na kikubwa wanahitaji pointi tatu. 

Nsajigwa alisema, wanaiheshimu Ndanda lakini hawataziacha pointi tatu hizo ili kuhakikisha wanautetea ubingwa wao wa ligi kuu msimu huu. 

Aidha amesema, wamefanyia marekebisho baadhi ya upungufu waliouona katika mechi zilizopita za ligi ili wapate matokeo mazuri.                      

Aliongeza kuwa, haitakuwa mechi nyepesi kwao kwani mara kadhaa timu yoyote inapokutana na mabingwa wanapambana ili kuifunga.                        

 Timu inaingia kambini leo jioni saa kumi na moja Izombe Hotels iliyokuwepo Kariakoo jijini Dar.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic