September 28, 2017




Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, iliyoketi hivi karibuni imepitia taarifa mbalimbali ya michezo iliyofanyika ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza na kufikia uamuzi ufuatao.

Kamati hiyo maarufu kwa jina la Kamati ya Saa 72, imepitia mchezo namba 18 (Majimaji v Yanga).

Mchezaji Salamba wa Majimaji kutokana na kumpiga mwenzake kiwiko amesimamishwa na suala lake linapelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Uamuzi wa kumsimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.

  
Katika mchezo huo Mwamuzi Msaidizi Namba Moja, Bw. Hassan Uhako kutoka Arusha hakuwa makini, hivyo kutomuona mchezaji wa Majimaji, Juma Salamba jezi namba 12 aliyempiga kiwiko mchezaji Emmanuel Martin wa Yanga na kumsababishia maumivu hadi kupoteza fahamu.

Kutokana na kitendo hicho Kamati imeelekeza Mwamuzi Msaidizi huyo ameandikiwa barua ya Onyo Kali kwa kukosa umakini. Adhabu hiyo dhidi ya Mwamuzi huyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic