September 28, 2017




Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, iliyoketi hivi karibuni imepitia taarifa mbalimbali ya michezo iliyofanyika ya Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza na kufikia uamuzi ufuatao.


Mechi namba 22 (Stand United v Singida United). 
Kocha wa timu ya Singida United, Hans van der Pluijm amepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuingia katika vyumba vya wachezaji na kutoa maelekezo wakati akiwa anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu aliyopata msimu uliopita akiwa na timu ya Yanga.

Adhabu dhidi ya Kocha Pluijm imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.


Mmiliki wa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ameandikiwa barua kwa uwanja huo kukosa maji ya bomba na badala yake kutumia maji ya kwenye ndoo au madumu hali hiyo ambayo inahatarisha afya za wachezaji.

1 COMMENTS:

  1. Hili la maji ya bomba mbona hata uwanja wa Taifa kuna wakati yanakosekana?Cha msingi ni kila anayehusika mahala popote atimize wajibu wake,kila kitu kitakaa sawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic