September 27, 2017


Huku wikiendi kwa mara ya kwanza kikitarajiwa kucheza nje ya uwanja wake wa Azam Complex, Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania, amefunguka kuwa hana wasiwasi wowote na michezo ya mikoani kutokana na kujiandaa nayo kwa muda mrefu na tayari ana dawa ya kushinda kwenye michezo hiyo.

Azam leo Jumatano wanatarajia kusafiri kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya kucheza na kikosi cha Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Hii ni mara ya kwanza kwa kikosi hicho kwa msimu huu kucheza nje ya Dar baada ya kupita michezo yao minne.

Kocha huyo amesema kuwa alijiandaa mapema kwa ajili ya mechi hizo kutokana na kutambua matatizo mengi yaliyopo ikiwemo sehemu mbovu ya kuchezea ambayo inafanya baadhi ya timu kushindwa pointi.

“Najua naenda ugenini, lakini sina wasiwasi hata kidogo kwa sababu tulishajiandaa tangu awali kwa ajili ya kucheza kwenye viwanja vya mikoani, na imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri kwenye mechi hizo kama ambavyo tulifanikiwa kupata pointi kwenye mechi za uwanjani kwetu.
“Unajua tangu zamani nilijua kwamba viwanja vingi vya mikoani havina ule ubora wa hapa kwetu, hivyo nilishaandaa mbinu na niliwapa mafunzo wachezaji wangu za kucheza kwenye viwanja hivyo,” alisema kocha huyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic