September 29, 2017



Huku kikosi cha Simba kikiwa katika maandalizi yake ya mwishomwisho kuelekea mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United, kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog amekuja na mbinu mpya itakayomwezesha kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, utafanyika keshokutwa Jumapili katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

 Omog amesema kuwa baada ya kuzikosa pointi tatu dhidi ya Mbao FC, sasa anatarajia kutumia mbinu mpya katika mechi  dhidi ya Stand United ili kuhakikisha anapata ushindi.

Alisema katika mechi na Mbao FC alianza kwa kutumia washambuliaji watatu ambao ni John Bocco, Emmanuel Okwi pamoja na Nicholaus Gyan lakini katika mchezo ujao dhidi ya Stand United, anatarajia kutumia mbinu nyingine ambayo anaamini itampatia matokeo mazuri.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Stand United na matarajio yetu makubwa ni kuhakikisha tunapata pointi tatu.


“Mfumo huo utakuwa tofauti na ule nilioutumia dhidi ya Mbao ambapo nilianzisha washambuliaji watatu,” alisema Omog huku akisita kutaja aina ya mfumo huo utakaotumia katika mechi hiyo.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic