KOCHA
Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ameibuka na kusema mshambuliaji wake mpya,
Nicholaus Gyan raia wa Ghana, ni hatari na kuwa kasi yake itaongezeka zaidi
pale atakapozoea mazingira kwa kuzoeana na wenzake.
Gyan
alifanikiwa kutupia bao lake la kwanza katika timu hiyo kwenye mchezo wa
kirafiki dhidi ya Hard Rock ya Zanzibar, akiwa amecheza dakika 45 tu za kipindi
cha pili ikiwa ni siku chache baada ya kutua Bongo.
Gyan
amesajiliwa Simba kwa mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo ambapo
alitambulishwa rasmi katika Tamasha la Simba Day Agosti 8, mwaka huu kisha
alirejea nchini kwao kwa ajili ya kumalizia mkataba wake katika timu aliyokuwa
akiichezea.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Mayanja amesema, kutokana na kiwango ambacho Gyan
amekionyesha katika mechi aliyocheza inaonyesha mwelekeo mzuri mara baada ya
kuelewana na wenzake kikosini hapo.
“Gyan ni
hatari sana, huyu ni mchezaji mzuri kwa jinsi alivyocheza katika mechi ya leo
‘Jumapili’, naamini ataendelea kuwa vizuri zaidi mara baada ya kuzoeana na
wenzake.
“Lengo letu
msimu huu ni kuona tunafanikiwa kutwaa ubingwa mapema hivyo uwepo wa kikosi
kipana kutatusaidia kufanya vizuri zaidi kwenye ligi,” alisema Mayanja.
CHANZO: CHAMPIONI
CHANZO: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment