April 20, 2025

 


UONGOZI wa Klabu ya Singida Black Stars umebainisha kuwa utapambana kuwaondoa wapinzani wao Simba katika hatua ya nusu fainali ili kutinga hatua ya fainali ya CRDB Federation Cup.

Singida Black Stars, Aprili 14 2025 ilipata ushindi mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Kaseja kwenye hatua ya robo fainali iliyochezwa Uwanja wa Liti.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Singida Black Stars 2-0 Kagera Sugar watupiaji wa mabao wakiwa ni Victorien Adebayo dakika ya 11 na Jonathan Sowah dakika ya 66 yanaipa tiketi timu hiyo kukutana na Simba SC iliyowafungashia virago Mbeya City robo fainali.

Ofisa Habari wa Singida Black Stars amebainisha kuwa baada yakushinda mchezo huo wanatambua mshindani wao katika hatua ya nusu fainali atakuwa Simba hilo haliwapo presha wapo tayari kuwakabili.

“Mchezo wetu wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba hatuna hofu nao kwa kuwa kikosi kipo imara na wachezaji wanauzoefu mkubwa ambacho tunahitaji nikiona kwamba tunapata matokeo nakusonga mbele katika hatua ya fainali.”

Simba ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex hivyo wababe hawa wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara kwenye msako wa mshindi atakayetinga hatua ya fainali.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi hawa watacheza na JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani, mshindi wa mchezo huu atatinga fainali.

Ndani ya Singida Black Stars kuna mshambuliaji mwenye zali la kucheka na nyavu anaitwa Jonathan Sowa amekuwa na hatari ndani ya uwanja akifikisha mabao 11 ndani ya ligi ikiwa ni ingizo jipya dirisha dogo.


Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic