September 23, 2017


MPIRA UMEKWISHA
SUB Dk 90+2 Yanga wanamtoa Ngoma na anaingia Emmanuel Martin
SUB Dk 90+1 Abdul Hamis anaingia kwa Ndanda, anatoka Ayoub Masoud


DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Yanga wanagongeana vizuri kabisa lakini mwisho wanashindwa kuipenya ngome ya Ndanda
Dk 85 Ndanda wanafanya shambulizi jingine kali hapa, lakini mwisho ni goal kick
KADI Dk 83, Massawe analambwa kadi ya njano kwa kumlalamikia mwamuzi
KADI Dk 79, Raphael Alpha amelambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Jabir  Aziz
Dk 77, Ngoma anaingia vizuri, anaachia mkwaju mkali kabisa, kipa anadaka vizuri kabisa
SUB Dk 75, Ajib anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya


Dk 75 sasa zimebaki dakika 15 mpira kwisha hakuna mashambulizi makali sana
Dk 70, Tshishimbi anapata dhoruba kidogo, yuko nje anatibiwa
Dk 66 Ndanda FC wanafanya shambulizi hapa inakuwa kona. Wanachonga lakini inakuwa nyanya kwa kipa Youthe
KADI DK 64 analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Massawe
Dk 60, Tshishimbi anampa Ngoma pasi ya kisigino, anaachia Ngoma shuti kali, goal kick
SUB Dk 58 Upande wa Ndanda FC anaingia Ophen Francis anaingia kuchukua nafasi ya Nassor Kapama
Dk 55, Ngoma anaruka juu na kupiga kichwa kinagonga mwamba wa juu, goal kick
Dk 54, Yanga wanapata kona nyingine baada ya shambulizi, inachongwa na Juma Abdul, Ndanda wanaokoa


Dk 53, kona maridadi inachongwa, Tshishimbi anaunganisha vizuri lakini mpira unagonga mtambaa wa panya, goal kick
Dk 52, Kamusoko anaachia mkwaju mkali kabisa lakini kipa anaokoa na kuwa kona DK 50, Yanga wanajitahidi kufanya mashambulizi kadhaa ingawa bado hayajawa makali sana kwa kuwa Ndanda FC wako makini
SUB Dk 47, Rajab Zahir anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Kelvin Friday, ni mabadiliko ya beki kwa fowadi
Dk 46, Zahir anaingia vizuri lakini ni goal kick
Dk 45 mpira umeanza kwa kasi na Yanga wanapata kona, inachongwa Ndanda na kuwa kona tena, inachongwa Ndanda wanaokoa tena.

MAPUMZIKO
Dk 46 +2 Ajib anajaribu vizuri kabisa baada ya Yanga kugongeana vizuri lakini goal kick
DK 45+1 krosi safi ya Gadiel, Ngoma anaruka juu sana, anaupiga lakini hauna nguvu. Yuko chini inaonekana ameumia

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

Dk 44, mwamuzi Jonesia anamtoa nje Dante kwa kuwa na skin tight yenye rangi tofauti, akirekebisha atarejea
Dk 42, Ndanda wanajitahi kutaka kurejesha bao lakini hawana mashambulizi makali na mpira zaidi uko katikati ya uwanja
Dk 37, Raphael anaachia mkwaju mkali wa faulo lakini hakulenga lango


GOOOOOOOOO Dk 34, Ajibu anaunganisha krosi nzuri akiunganisha vizuri mpira wa Yondani
Dk 30, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini Juma Abdul anafanya kazi ya ziada kuokoa na kuwa kona. Yuko chini anatibiwa
Dk 27 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali sana
Dk 20, Zahir anafanya kazi ya ziada kuokoa miguuni mwa Kamusoko
Dk 18, Yanga wanachonga kona kupitia Juma Abdul, Ndanda wanaokoa hapa. 
Dk 17, Yondani anapanda na kugongeana vizuri na Chirwa, konaaaaDk 16, mpira bado haujachangamka sana na zaidi unachezwa katikati ya uwanja
Dk 12, Ajib anapokea pasi ya Raphael na kuachia mkwaju lakini hakulenga lango
Dk 11, Kapama anaingia vizuri karibu na lango la Yanga lakini shuti lake ni nyanya kabisa


DK 9, Majid Bakari analambwa kadi ya njano kwa kumpiga Yondani buti la tumbo 
Dk 5, Ndanda wanachonga kona yao lakini ni dhaifu inatoka nje
Dk 5, mwanuzi Jonesia anamtoa nje Yondani, inaonekana hakuvaa vizuri, soksi zake hazifanani na wenzake, atarejea akiwa amejirekebisha
DK 4, Ndanda wanafika kwenye lango la Yanga kwa mara ya kwanza na kupata konaaa
Dk 1, Kona inachongwa vizuri kabisa na Juma Abdul lakini Chirwa anabutua juuuu
Dk 1, mpira unaanza kwa kasi na Yanga wanaonekana kushambulia kwa kasi, Chirwa anaingia vizuri, kona

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV