September 22, 2017



Unaweza kusema sasa mambo safi kwa Diego Costa, kwani hatarejea tena Chelsea sehemu aliyosema asingependa kurejea.

Atletico Madrid ya Hispania na Chelsea zimekubaliana kuhusiana na uhamisho wake na sasa Atletico imekubali kutoa pauni million 57.5 kumrejesha mshambuliaji huyo kundini.

Mwaka 2014, Atletico ilimuuza Costa kwa pauni million 32 kwenda Chelsea na amekuwa na mafanikio makubwa.

Lakini ujio wa Kocha Antonio Conte ukageuka matatizo kwa Costa hasa baada ya kumtumia ujumbe kwamba “hamhitaji”.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic