Ruvu Shooting imecheza na Mtibwa Sugar na kuambulia sare ya bao 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Abdulrahm Mussa alimpa pasi Zuberi Dachi katika dakika ya kwanza tu akaandika bao.
Shooting walitawala kipindi cha kwanza wakiwahenyesha Mtibwa Sugar na walikwenda mapumziko wakiongoza 1-0.
Kipindi pili, Mtibwa Sugar walikuwa kama nyuki wakilishambulia lango la wenyeji wao kama “ugomvi” na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Stamili Mbonde katika dakika ya 55.
Kabla ya mechi hiyo, Masau Bwire ambaye ni Msemaji wa Ruvu Shooting, walionekana wakiwa katika pikipiki pamoja wamepanda “mshikaji” na Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru.








0 COMMENTS:
Post a Comment