September 24, 2017




Baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Milambo FC mjini Tabora, Simba itarejea mkoani Mwanza kuweka kambi.

Simba itaweka kambi mkoani Mwanza kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United, wikiendi ijayo.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wanaona Mwanza ni sehemu nzuri ambayo wanaweza kuweka kambi.

"Mwanza ni sehemu sahihi, tutaweka kambi pale. Tutajiandaa hadi siku tutakaposafiri kwenda Shinyanga kwa ajili ya mechi dhidi ya Stand," alisema.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic