September 8, 2017


TAARIFA za Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi, jana mkoani Dodoma zilifanya hata watu wa soka nao kuanza kujadili juu ya tukio hilo ambalo limemkuta mwanasiasa. 

Lissu ambaye aliwahi kuzungumza na Global TV na kukiri kuwa yeye ni shabiki wa Yanga ambaye hajawahi kwenda uwanjani tangu mwaka 1993, alikumbwa na tukio hilo majira ya saa 7:30 mchana nyumbani kwake eneo la Area D mara baada ya kupaki gari lake alipokuwa akitoka bungeni mkoani humo. 

Baada ya tukio hilo, haraka mwanasiasa huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu. 

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii mashabiki wengi wa soka walionyesha kushtushwa na kilichotokea hasa baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kukiri kutokea kwa tukio hilo, jana mchana na kusema Lissu alikuwa kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya matibabu zaidi lakini baadaye ilidaiwa kuwa alikuwa mbioni kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwenye Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. 

Maoni hayo yaliyotolewa kwenye kurasa za Instagram, Facebook na makundi ya WhatsApp yalikuwa yakikinzana ambapo wapo waliohisi ni sababu za kisiasa huku wengine wakisema inaweza kuwa mambo binafsi. 

Katika mahojiano yake, aliyofanya kuhusu soka, Lissu alisema yeye ni shabiki wa Yanga lakini mara ya mwisho alipokwenda uwanjani alibebwa juujuu na kutaka kuvuliwa suruali na mashabiki wa Simba, katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya Stella ya Ivory Coast, hivyo tangu siku hiyo hajawahi kwenda tena.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic