September 21, 2017




FULL TIME
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Kipa wa Mbao FC anadaka vizuri shuti la faulo
KADI Dk 88,Mohammed Kassanga wa Mbao analambwa kadi ya njano kwa mchezo wa kibabe, Simba wamepata faulo nje kidogo ya lango la Mbao FC

Dk 86, Maganga tena anaachia mkwaju mkali sana hapa, Manula anadaka vizuri
Dk 83 Simba wanafanya shambulizi kali kabisa lakini Mbao FC wanaonekana wako makini kabisa

GOOOOOOOOOOOOOOO Dk 81 Emmanuel Mbuyokole anaifungia Mbao FC bao bora kabisa la kusawazisha
Dk 80 sasa, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja na Simba ndiyo wanaoumiliki zaidi na Mbao FC wakijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza
SUB Dk 75 Juma Liuzio anaingia kuchukua nafasi ya Nicholas Gyan

Dk 74, Mbao FC wanafanya kazi ya ziada kuokoa mpira miguuni mwa Okwi
Dk 69, Niyonzima anaachia mkwaju mkali kabisa nje ya 18, goal kick
Dk 67, Simba wanafanya shambulizi kubwa lakini shuti la Okwi linapaa juu
Dk  65, krosi nzuri ya Niyonzima, Bocco anaruka lakini kipa anauwahi
Dk 65, Niyonzima anaingia vizuri anachambua Mbao wanaokoa na kuwa kona


SUB Dk 64 Ibrahim Njohole anaingia anatoka Emmanuel Mbuyokole upande wa Mbao FC
Dk 61, Okwi anaingia kwa kasi na kuachia krosi safi kabisa, Mbao wanaokoa kwa ustadi wa juu
SUB DK 59 Mbao FC wanamtoa Moses Shabani anatoka anaingia Ndani Kisambala
Dk 58, Okwi anaachia mkwaju baada ya Simba kugongeana lakini hakulenga lango
Dk 57 sasa, mpira unachezwa katika ya uwanja zaidi, Simba wakiwa wanatawala zaidi
Dk 54, Mbao FC wanafanya shambulizi na kupata kona, inachongwa hapa, Manula anaokoa lakini inaonekana aligongwa
Dk 53, Okwi anaingia vizuri na kuachia mkwaju mkali, unapita juu kidogo

Dk 50, Simba wanapata kona baada ya kushambulia lakini Mbao wanaokoa
GOOOOOOOOOOOOOOO Dk 47, faulo ya Nyoni, Kotei anaunganisha vizuri kabisa na kufunga bao la pili
Okwi anaingia vizuri, anaachia shuti kali na kipa anaokoa vizuri
GOOOOOOOOOOO DK 46 Habibu Haji anaachia shuti kali kabisa linalomshinda Aishi Manula

Dk 45, Mbao wanaonekana kuanza kwa kasi sana 

MAPUMZIKO
Dk 45 + 4 Niyonzima anaingia kuchukua nafasu ya Kichuya aliyeumia

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 45 Moses Shabani wa Mbao na Juuko Murshid wanalambwa kadi ya njano kwa kusukumana
Dk 43, Mbao wanaanza kucheza kibabe
Dk 40, Okwi anapiga mkwaju wa adhabu unapita juu kidogo ya langoKADI Dk 39  Ndikumana analambwa kadi ya njano kwa kumkwatua Bocco
SUB Dk Mbao FC wanafanya mabadiliko, wanamtoa Hebert Lukindo anaingia Said Said
Dk 34, Simba wanapata kona, Muzamiru anaachia shuti kali kabisa hapa lakini goal kick
DK 32 mpira umesimama kwa muda, kuna mchezaji wa Mbao FC anatibiwa


Dk 30, Gyan anaingia vizuri lakini anashindwa kuwa na kasi, Mbao FC wanaondosha
Dakika ya 25: Juuko wa Simba analalamika kwa mwamuzi.
Dakika ya 24: Kuna wachezaji wawili wa Mbao FC wanapasha misuli, shangwe ni nyingi kwa mashabiki wa Simba.
Dakika ya 20: Simba wanaongeza kasi ya kushambulia.

Dakika ya 17: Mashabiki wa Simba wamenyanyuka wanashangilia kwa shangwe nyingi.

Bao hilo limeingia kwa kichwa.

Dakika ya 16: Simba wanapata bao la kwanza, mfungaji akiw ani Shiza Kichuya, amefunga baada ya kupata pasi kutoka kwa Erasto Nyoni upande w akulia.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO


Dakika ya 14: Okwi na Nyoni wanacheza pasi lakini wanarudisha nyuma.


Dakika ya 11: Mbao wanafanya shambulizi kali lakini mpira unatoka nje.

Dakika ya 7: Simba wanatengeneza mashambilizi lakini bado mambo ni magumu.

Dakika ya 4: Timu zote bado zinasomana.

Dakika ya 1: Mchezo umeanza ka kasi ya taratibu.


Mwamuzi anaanzisha mchezo.

Timu zinaingia uwanjani kuanza mchezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic