September 10, 2017

Baada ya tetesi za hapa na pale hatimaye imethibitishwa rasmi kuwa Said Ndemla amepata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Sweden.

Meneja wa mchezaji huyo wa Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Jamal Kisongo amesema kuwa ni kweli Ndemla amepata nafasi hiyo lakini kikwazo kikubwa kwa sasa ni Visa ya kuingia na kufanya kazi nchini Sweden ndiyo ambayo bado inasumbua.

Kisongo amesema kuwa Ndemla amefuzu majaribio yake ambayo alienda mara ya kwanza na wao wapo kwenye mchakato wa kutafuta Visa ya kumwezesha kukamilisha uhamisho wake ili akacheze soka la kulipwa.

“Bado suala la Visa ni tatizo lakini tunalifanyia kazi, Ndemla ni mchezaji mzuri na mimi ni mmoja wa mashabiki wake, amekuwa akionyesha uwezo mzuri uwanjani.

“Kuhusu suala lake tutaenda TFF wakatusaidie, nitamfuata katibu wa TFF atusaidie juu ya suala hilo na pia serikali inaweza kuingilia kusaidia ili kufanikisha mchakato wa kupata vibali, unajua timu ambayo anatakiwa kwenda Ndemla ni ile ambayo alikuwa akiichezea Thomas Ulimwengu.”

1 COMMENTS:

  1. Kwani Thomas hayupo tena kwenye hiyo timu?
    Na suala lake mbona limechelewa hadi transfer window ishafungwa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic