Cristiano Ronaldo ameichezea Real Madrid mechi ya 400 leo wakati timu hiyo ikiivaa Borussia Dortmund ya Ujerumani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tokea ametua Madrid akitokea Manchester United tayari Ronaldo ameichezea Madrid mechi 267 za La Liga.
Pamoja na mechi hizo za La Liga, amecheza mechi 30 za Copa del Rey na mechi 90 za Champions League ikiwemo ya leo.
Mechi nyingine sana ni za Supercopa de Espana, mvili za European Super Cup na nne za FIFA Club World Cup.
Tokea kuanzisha kwa Madrid ambayo ni moja ya klabu kongwe Ulaya na duniani kote ni wachezaji 22 tu walioweza kufikisha mechi 400.
Gwiji la Real Madrid, Raul Gonzalez ndiye anashika namba moja baada ya kuichezea timu hiyo mechi 741 katika michuano yote.
Kwa upande wa Ronaldo, sasa anakuwa mchezaji mgeni wa tatu kucheza mechi nyingi na Real Madrid baada ya beki Mbrazil, Roberto Carlos aliyefanikiwa kucheza mechi 527 na beki mwingine Mbrazil ambaye bado anacheza, Marcelo aliyefikisha mechi 416.
0 COMMENTS:
Post a Comment