September 19, 2017


Kikosi cha Simba kimefanya mazoezi yake ya kwanza leo kwenye Uwanja wa Alliance uliopo eneo la Mahina jijini Mwanza.
Simba iko jijini humo kwa ajili ya mechi yake ya kesho dhidi ya Mbao FC itakayopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Kikosi cha Simba kimetua Mwanza kikiwa na watu 24 ambao wanajiandaa na mechi hiyo dhidi ya Mbao FC.
Tokeo msimu uliopita, Simba na Mbao FC zimekuwa na upinzani mkubwa zinapokutana.

Mechi ya mwisho ilikuwa ni ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na Simba ikashinda kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic